💡💡KWANINI HAWAFANIKIWI WAKIWA VIJANA 🤔🤔

 🔮🔮🔮

💡💡💡

Hili limekua swali langu, ambalo nimekua nikijiuliza mara nyingi saana na sikuwa napata majibu.

Lakini nilipo endelea kujitathimini mwenyewe, kuna mambo ambayo nimeanza kujifunza. 

Nadhani hata wewe utakua shahidi ya kwamba asilimia kubwa ya sisi vijana, watanzania, ni vigumu saana kumkuta kijana wa miaka 20 - 30 anamiliki mali za kutosha kiasi kwamba tumuite tajiri.

Japo kwa sasa kumeanza kutokea mapinduzi, hatimae vijana wamekua na nafasi kubwa na kuwa katika orodha ya matajiri wanao chipukia.

Lakini leo natamani nikushirikishe mambo ambayo yanawarudisha nyuma vijana wengi na kufanya wakachelewa kuyafikia mafanikio yao.

📅📝

💡💡


1. Vijana wanataka maendeleo yalio tayari.

Ni wazi kwamba vijana tunapenda saana maendeleo, lakini tumeshindwa kua chachu ya maendeleo yenyewe.

💡

Huwezi fikia uchumi mkubwa kama utategemea mtu frani afanye jambo harafu wewe uende kufanya akiwa tayari amelifikisha mahar frani.

Point yangu ni hii. Kijana kua mbunifu, na tafuta namna ya kuitatua hiyo changamoto ulio nayo sasa. Wewe ndio uwe msaada wa kutatua changamoto za wengine.

💡💡🕯

💦💨

02. Kushindwa kabra ya kushindwa.

Kuna vijana huwa wao wanashindwa jambo hata kabra ya kushindwa, yaan mtu anashindwa jambo kabra ya kuanza kulifanya.

Huo ni uvivu, huwezi kufanikiwa kamwe kama utalitazama jambo kwa macho na kusema huwezi nila kulijaribu kufanya. 

Ukitaka mambo yako yaende kataa neno "SIWEZI" labda iwepo sababu ambayo iko juu ya uwezo wako ambayo itakufanya ushindwe kulifanya hilo jambo. Ila usiache kuthubutu hata kama ulifeli mwanzo.

💡💡

💨💦

03. Kukosa taarifa sahihi.

Huwezi kufanya jambo lolote likafanikiwa kama huna taarifa sahihi kuhusu jambo hilo. 

💡

Jambo la muhimu, tafuta watu muhimu ambao unajua watakufaa kufika mahari unataka kufika, 

Pata taarifa sahihi kuhusu jambo unalotaka kufanya utafanikiwa.


💦💨

🔮🔮

💡💡💡

Kumbuka kipindi sahihi cha kujenga na kuinua msingi wa uchimi wako ni sasa, huu  ndio wakati unaweza fanya lolote na likafanikiwa.

Kipindi cha ujana ndicho kinaamua wewe utakua mama au baba wa aina gani, ndicho kipindi ambacho kinatoa picha ya wewe utakua na familia ya aina gani.

Usishindwe kabra ya kushindwa, na ukiona unashindwa usikubali kushindwa, ilimradi hilo jambo ni jema.

Unaweza kuwa vyovyete na kumiliki chochote.

Be you

We're tomorrow builders

@yusuph kapusi

💡💡💡💡💡💡

Comments